Jela Lyrics
Daddy naiandika barua
Nina imani itakufikia
Mi mwanao naumia
Majukumu uloniachia
Mama naye kafariki ee
Wadogo zangu nitawaleaje?
Hata shule nimeshindwa mie
Mawazo kichwani mi nawazaje
Kwanza kosa ni nini daddy
Lilo kufanya uende jela?
Nasikia tu majirani
Wengine wanasema eti uliua
Kama unavyojua, umri wangu mdogo
Mdogo na nategemewa
Majukumu ni mengi
Ni mengi na naelemewa
Daddy ni lini utatoka jela
Uje umwone Khan na Nilima
Leo hatuna hata pa kulala tunaumia
Daddy ni lini utatoka jela
Uje umwone Khan na Nilima
Leo hatuna hata pa kulala tunaumia
Sillah, oooh barua yako nimeipata
Eh eh eh musilie mwanangu (Nyamaza)
Usijali nitatoka (Nyamaza)
Tazama wadogo zako na uwatuze (Nyamaza)
Karibu nitarudi (Nyamaza)
Mwambie jirani yetu Mama Shufa(Nyamaza)
Awape hata uji (Nyamaza)
Na kama mkishindwa nendeni mkaombe ila msiibe
Kimeniumiza sana kifo cha mama yako
Ingawa sijui chanzo ni nini
Chanzo ni nini
Okey soma mwanangu usiache shule
Soma mwanangu nakutegemea wewe
Mwanangu wee, we ndo kidume
Nakusisitiza ndugu zako watunze
Na kuhusu kosa langu la mi kuwa jela
Ukikuwa utajua
Mtoto wa kiume simba hafundishwi kuwinda
Hivyo najua utashinda
Kwaheri wasalimie wenzako
Waambie nawapenda nitarudi nyumbani
Tuishi kama zamani, zamani
Kama unavyojua, umri wangu mdogo
Mdogo na nategemewa
Majukumu ni mengi
Ni mengi na naelemewa
Daddy ni lini utatoka jela
Uje umwone Khan na Nilima
Leo hatuna hata pa kulala tunaumia
Daddy ni lini utatoka jela
Uje umwone Khan na Nilima
Leo hatuna hata pa kulala tunaumia
Sillah, oooh barua yako nimeipata
Eh eh eh musilie mwanangu (Nyamaza)
Usijali nitatoka (Nyamaza)
Tazama wadogo zako na uwatuze (Nyamaza)
Karibu nitarudi (Nyamaza)
Mwambie jirani yetu Mama Shufa (Nyamaza)
Awape hata uji (Nyamaza)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Jela (Single)
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE