Mama Lyrics
Kama isingekuwa wewe mama
Maisha yangu yasingekuwepo
Kama isingekuwa wewe mama
Maisha yangu yasingekuwepo
We ndo ishara ya ushindi mama
Umenilea kwa misingi mama
Miezi tisa tumboni uko nami
Kwenye mvua na jua uko nami
Usiku wa kulala ukakesha uko nami
Ukalala njaa ukashiba uko nami
Nakuomba Mungu baba tazama (pekee yake pekee)
Umlinde usiku mchana wangu mama (Akulinde nawe mwanangu)
Aliyekupenda kila jua likizama
Akikupenda mama pekee ni karama
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Fanya kazi kwa bidii mwanangu
Unitunze mama yako mwanangu
Saidia kila mtu mwanangu
Mungu akupee imani mwanangu
Ooh mwanangu jaribu
Kutofautisha wabaya na wema
Hakuna wa kukuhangaisha
Hata kama wanasema
Umtunze baba yako
Uwalee ndugu zako
Wapende jirani zako
Uzipate radhi zako
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Aaah aah mamaa, mama
Khadija Kopa na Mwanawe ndogo Janja eeh
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Asante Mama (Album)
Copyright : (c) 2021 MMB (Manzese Music Baby)
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE