Home Search Countries Albums

Confession Of A Mad Son

DIZASTA VINA

Confession Of A Mad Son Lyrics


Ah! watakwambia mi’ wa kishua ‘cause I’m cute and
Niko juu kama human kwenye food chain
Vile I look good and I got this cool slang
Na nina rap skills ka’ Sean P wa Boot Camp
Watasema kuhusu my intelligence my balances
Watakuambia kuhusu my Teammates my Alliances
Watakuambia kuwa nina fans mpaka Kansas
Na nina-ball pia nina-draw pia ni Enthusiast wa Science
Watakuambia kuwa nina fans mpaka Marabu
Watakuambia kuwa my brain is all lava-full
Watakuambia kuwa nina perfume
Ninayopaka kuwa ina karafuu na ina-smell wonderful
Hawatakuambia kuhusu aliyenikanya hadi nikome
Aliyenizaa akanilea akani
Akanipenda, akani
Akanifanya msafi mnione
Silabi, ah! zinaunda vitenzi kwa irabu
Kutengeneza mashujaa wengi wa vitabu
Tarihi zinatungwa toka enzi za mababu
Mi’ nimeona shujaa wa kweli ni ajabu
Sidhani, kama inatosha kusema “thank you”
Ukinihitaji just whistle and ‘Imma’ rescue
Ni bahati leo niko hai, simple nafurahi kukuona
Ukiwa happy and I’m grateful
Kama nina nyota nyumbani nahitaji nini?
Nahitaji nini?
Uko moyoni mahala ambapo nahifadhi pin
Naku-post ‘Insta’ kisha naku-hashtag #queen
Wapo ambao walifuga kiburi
Wakazipanda mbegu wakavuna sifuri
Walichana misamba wakavunja misuli
Sikutetereka maana ulinifunza vizuri
Umenifunza jinsi ya kuishi na pia
Umenipa hekima umenipa misingi na njia
Kisha ukanipa bega kubwa la kukidhi dunia
Linanipa faraja pindi n’napohisi kulia
Nani mjinga azuie mbegu bora kuchipua?
Labda kama shamba limezongwa na mabua
Umenilea ‘Soja’ nimekua, umenifunza akiba
Maana umasikini kidonda natambua
Niko mbali natafuta miradi sawia
Mvua inanyesha radi nasikia,
Bado nasimama Imara, Asante kwa kunilea vyema mama
Umeipa zawadi dunia
Asante kwa upendo wako asante kwa kunipatia hifadhi
Asante kwa mabusu siwezi kuhesabia idadi
Asante kwa picha kali naiandikia dibaji
We’ ni shujaa nitasimulia vizazi
Happy Birthday
 
Happy birthday
Happy birthday
Happy birthday

Ukubwa wa upendo wako hauwezi wekwa mchanganuo
Nimekulia mahala ambapo kuwa mwema si chaguo
Umenipa busara sihitaji tena mafunuo
Ikiwa nimepewa funguo, ya kuifungua dunia
Nasikitika kauli yangu sio rasmi
But I’m sure you’ve always meant for some’ high
Maybe that’s how Angel got to be
You’re a proven God to me
Wimbo huu ni upendo wangu kwako
Marafiki wanafurahia uwepo wangu japo
Wapo kadhaa wanaochukia uwezo wangu
Hawatajua wala kuikisia kesho yangu
We’ ni kioo naona kesho nai-reflect vile
Naona pande naona mbele najiuliza
Mi’ ni nani nikusahau nikudharau
Wakati wazi umenipa sababu moja zaidi ya ku-respect women
Siwezi lipa tone la kamasi ulilonifuta
Siwezi tafuta chozi la samaki lililovuja
Siwezi badili muda kisha ukawa thamani
Nikaurudisha nawakusanya wenzangu nawafundisha
Tumweshimu mama, wapi tunda pasipo mbegu?
Imeandikwa iwapi rutuba pasipo nyevu
Usipojua umuhimu wa msingi kwa kuta ndefu
Ni sawa na kuzipanda mbigiri na kuja peku

We’ ni sauti ya uchochezi, hasa n’napolega
We’ ni lugha we’ ni kurasa yangu pendwa
We’ ni kitabu kitamu siwezi weka kando nikishika
We’ ni ka’ kiini kwenye Atom
We’ ni Oprah, Michelle, Shyrose Bhanji
We’ ni Winnie Mandela, Sophia (sonia) Ghandhi
We’ ni kama paka mwenye roho tisa
We’ Serena, we’ ni Stosh Fellie, Go  Tifa
You’re my Violet my Rose and my lily ah!
You’re my best friend, you’re my wishing star
You’re my sweet dreams my wonder woman
My Cat woman, my first love and that’s vivid
You love when I’m broke and when I get paid
Before and after my payday
You love me anyway, so I surrender my Ego
And my Arrogance and I’m singing happy birthday

Happy birthday
Ohh Happy birthday
Happy birthday
Happy birthday

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2022


Album : Confession Of A Mad Son (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

DIZASTA VINA

Tanzania

Dizasta Vina  (real name Edger Vicent) aka "The Black Maradona" is  Hip-hop arti ...

YOU MAY ALSO LIKE