Home Search Countries Albums

Mwaka Wangu

BEATRICE MWAIPAJA

Mwaka Wangu Lyrics

Wakati wa kulima mi nililima kwa maumivu
Hata niipopanda ilibidi kusubiri 
Hata niipopanda ilibidi kusubiri 

Nilisubiri kwa maumivu mi nilingoja
Nilisubiri sikusahau kumwagilia
Mi nilisubiri sikuwacha weka mbolea 
Leo ni mwaka wangu, mwaka wangu wa neema

Leo, leo subira imevuta heri
Leo, leo ni siku yangu aha

Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa heshima yangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa baraka yangu, mwaka wangu wa mavuno

Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa heshima yangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa baraka yangu, mwaka wangu wa mavuno

Nayaona mema kwa maisha yangu nayaona
Maandiko yamesema aonavyo mtu ndivyo alivyo
Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa heshima
Huu ni mwaka wangu, ni mwaka wa urejesho

Vilivyoliwa na nzige na tunutu vinarudishwa
Ile heshima niliyoikosa naipata
Maana huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa heshima
Kila apandacho mtu atavuna

Nilipanda kwa maumivu leo navuna kwa furaha 
Ile miaka iloliwa na nzige na tunutu wee
Bwana anairudisha tena double double
Mwaka wa kumiliki, mwaka wa kutawala

Mwaka wa heshima 
Mwaka uliokubalika na Mungu kwangu ndio huu
Mimi ni mwaka wangu tena mwaka wangu
Mwaka wa urejesho ooh

Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa heshima yangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa baraka yangu, mwaka wangu wa mavuno

Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Huu ni mwaka wangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa heshima yangu, mwaka wangu wa mavuno
Mwaka wa baraka yangu, mwaka wangu wa mavuno

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG

Release Year : 2021

Album : Mwaka Wangu (Single)

Copyright : (c) 2021

Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

BEATRICE MWAIPAJA

Tanzania

Beatrice Mwaipaja is an Activist for Jesus, Gospel Artist from TANZANIA, Wife and a  Songw ...

YOU MAY ALSO LIKE