Home Search Countries Albums

Kuchagua

BABA SILLAH

Kuchagua Lyrics


Ni kama hadithi fulani
Ilonikuta maishani
Kipindi nasaka mwendani
Kupendwa na ndugu wawili

Mara kwanza kukutana naye
Nikampa namba ili na ajitwange
Cha ajabu akanishushua
Na kuniona sina dhamani ya kuwa naye

Nikihisi nyota ilififia
Nikajiona sina dhamana
Mara Mola akanishushia 
Aliyefanana nayeye

Sikuamini ule usiku wa saa sita
Message kuingia
Yule wa kwanza aliyegoma 
Kwa sasa kanikubalia 

Sikuamini ule usiku wa saa sita
Message kuingia
Yule wa mwanzo aliyegoma 
Kwa sasa kanikubalia 

Nimeshindwa kuchagua
Nimpende nani nimuache nani
Yule ananiita baby
Huyu ananiita hunnie

Na tena ni ndugu wa damu
Huwezi amini mapacha wanaofanana
Mwenzenu nakosa hamu
Yalonikuta nakosa la kufanya

Usoni kijasho chembamba
Kinanitoka toka
Wakiwa wote wakiniita
Mi naogopa ogopa

Na kwenye jangwa mi nimenasa mie
Yupi nimpende na yupi nimwachilie

Sikuamini ule usiku wa saa sita
Message kuingia
Yule wa kwanza aliyegoma 
Kwa sasa kanikubalia 

Sikuamini ule usiku wa saa sita
Message kuingia
Yule wa mwanzo aliyegoma 
Kwa sasa kanikubalia 

Nimeshindwa kuchagua
Nimpende nani nimuache nani
Yule ananiita baby
Huyu ananiita hunnie

Nimeshindwa kuchagua
Nimpende nani nimuache nani
Yule ananiita baby
Huyu ananiita hunnie

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Kuchagua (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

BABA SILLAH

Tanzania

BABA SILLAH aka Bongo Rider is an artist from Tanzania. He is the father of Khan Sillah and Dogo Sil ...

YOU MAY ALSO LIKE