Ni Ngozi ya Mwafrika Lyrics

Ah mama mamama ma Miriam Makeba
We mama mamama ma Rebecca Malope
Rose Muhando, Yvonne Chaka chaka
----
----
Naazimia moyoni mwangu nitatoka hapa
Maana maisha ya nyumbani yamenishinda
Najiuliza naumiza kichwa mimi niende wapi?
Maana bado ngozi ya Muafrika ina shida
Mbona nakuwa mtumwa?
Katika nchi zile za ugenini
Mwafrika?
Mwafrika nina nini?
Mbona mnanionea?
Nikiwa katika nchi za ugenini
Mbona mnaninyanyapaa
Ngozi yangu ina nini?
Mbona mnanidharau
Mwaniita nyani
Eti mwafrika ni tumbili
Eti hatuwezi kujiongoza wenyewe
Mwafrika nina nini?
Nimewakosea nini?
---
---
Mlikuja kunitawala bila hiari
Nikawa mtumwa wenu Mwafrika
Nilipoomba uhuru wangu Mwafrika
Mkaniua bila huruma
Damu likamwagika Afrika
Mwafrika nina nini?
Nimewakosea nini?
Pole mwafrika
Unatumia vibaya
Unadanganywa toto mwafrika
Wachukue mali zako
Wanakuletea magonjwa mwafrika
Tena wanaletewa madawa Afrika
Unadanganywa toto mwafrika
Wanapenda uwasujudie mwafrika
Wanatugombanisha waafrika
Ili tuuwaane waafrika
Ili wachukue mali zetu waafriaka
Mwaafrika uko wapi?
Rudi nyumbani mwafrika
Acha kuhangaika kwa watu mwafrika
Njoo uinue uchumi wa nchi yako mwafrika
Rudi nyumbani mwafrika
Njoo uijenge nchi yetu mwafrika
Mwafrika, rudi nyumbani mwafrika
Huko sio kwenu mwafrika
Mbona umevamia ya watu mwafrika
Ushoga sio wetu mwafrika
Usagaji sio wetu mwafrika
Rudi nyumbani mwafrika
Umeharibika mwafrika
Umesahau maadili mwafrika
Unaiga ya watu mwafrika
Rudi nyumbani mwafrika
Mwafrika wewe...
---
---
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Ni Ngozi ya Mwafrika (Single)
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE