Home Search Countries Albums

Wamechoma Moto

AMBWENE MWASONGWE

Wamechoma Moto Lyrics


Nilikuta mtu amelala kakauka
Anafuka moshi, wamemchoma moto
Kila nikikumbuka thamani ya mtu bado moyo wanhu wauma
Waliozunguka ule mwili wengi, walitema mate na kushangilia
Nikasikia maneno amekoma, wanatusumbua sana
Nikawaza angekuwa mwanangu
Nikawaza, angekuwa ndugu yangu
Nikawaza, ningekuwa mungu wake
Maumivu yangekuwaje?
Nikatamani nimnon’oneze
Nimuulize, nini kimemkuta?
Bahati mbaya hawezi sikiaaaa, amekufa kwahuzuni
Nikamkumbuka mama yake nyumbani
Kapokeaje taarifa hizi mbaya
Bahati mbaya, liliumaje kuletewa maiti ya mwanawe
Nikamkumbuka mungu amejisikiaje
Mwanadamu aliyeumbwa kwa ajabu na kutisha
Ndipo, nikamchukia shetani
Anavyitafuna maisha ya watu eeeh eeeeh
Bwana yakumbuke maneno, yale ya mwisho
Waliolia wakijuta, wanapokufa
Kumbuka ile hali ya kupoteza
Maisha ukarehemu ukawasikie

Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe

Wananyongwa kwa ubaya
Wananyongwa kwa aibu
Wanamezwa na dunia wanapotea aaah
Magonjwa laana shida mateso
Vinawatafuna hawaelewi
Wanahitaji msaada wako
Wanahitaji huruma ya kwako
Maana ni ya kwako uliwaumba uliwafanya aaah
Shetani kawadhulumu maisha
Wakiitaji msaada, bwana ukawajibu
Katazame machozi na damu walizomwaga  ukawakumbuke
Kama hautawahurumia wao basi
Hurumia wanaowategemea eeeh
Hurumia wanaoumizlzwa na matendo yao
Bwana ukawarehemu
Kama ukiwatupa wewe unamtupia nani
Kama ukiwageuzia kisogo waende kwa nani
Maana kwako ndiko kuna wema
Wewe ni mungu wa kusamehe
Bwana ninawaombea watu

Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Wakiita aaah uwasikieeee
Ukakumbuke wema  wa kwako mwenyewe
Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2022


Album : Wamechoma Moto (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

AMBWENE MWASONGWE

Tanzania

Ambwene Obadia Mwasongwe  is a gospel artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE