Ruge Lyrics
Sijawai muona na upara, punk, dredi kama Chege
Hajawai vaa skin tight, Jeans shusha mlege
Sijui fegi, bangi, shisha, henny, mbege
Busara kila neno alikuwa habongi kibwege
Alikuwa mbongo clever, Kwaya, mixer reggea
Mzalendo kweli kweli ngangaro si legelege
Mamalkia wa nguvu, vipepeo kedekede
Kapromote michezo labda kama hukua ready
R.U.G.E jina lake Ruge
Alama alizoacha ni sifa tusizuge
Kama taifa lazima nyufa tuzibe
Usije dondoka ukuta uwazi vyetu waibe
Aliamini sanaa, wasanii na bidhaa
Kwanza pata nafasi, jenga jina kuwa star
Ongeza dhamani na nidhamu kwa mitaa
Maintain status ndio business na chapaa
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze
Maneno yenye nidhamu kwa saiti ya upole
Bila kulipa ada wengi tulipata shule
Kwa makelele ya shangwe kama fiesta
Aliona upande wa pili vipi wakitambua na fursa
Mdogo mdogo vijana wakapigwa msasa
Bila kubagua dini, jinsia au siasa
Ogopa Mungu na technologia
Hicho ndicho ambacho alicho tuhusia
Najua wengi tu wameshakuimbia
Wengine wana mengi wanataka kukuambia
Ila ndo umeshatangulia
Nenda, jasiri muongoza njia
Scofield, Big Joe anagugumia
CMG kila siku twakuombea
Yeah, najua tunafatia salam
Kwa uncle KIBS zizi na kuendelea
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Alikuwa ni baba
Alikuwa mwalimu kwetu
Alisimama kama nguzo yetu
Alikuwa ni baba
Alisimama kama nguzo yetu
Lets take over the game
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Ruge (Single)
Copyright : All rights to the owner.
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE