Home Search Countries Albums

Sinaga Swagga 5

YOUNG KILLER MSODOKI Feat. DIPPER RATO

Sinaga Swagga 5 Lyrics


Mwenzako akinyolewa nawe tia maji usikejeli
Hasa ndo nimeanza kuifanya kazi kweli kweli
Toa mjukuu mwenye nyumba katimba mpaka mpaka haalikwi
Yaani mjenzi kapatikanika kwenye miti
Suka gombanii siti baba haringishiwi pipi
Kiziwi akiamua kuchana hazingatii beat
Huwezi kukatari alafu baadae uombe dua
Kubomoa nyumba ati kisa redio inazingua
Uh it was a dream now its my real life

Yaani quality alafu haraka utadata shenzi type yoh
Usiparamie lichocho utatamani kupaa 
Yoh bora usipike mawe utaharibu mkaa 
Haina haja ya kuleta jam jam zama hizi
Kumwambia nyani asali ni tamu kuliko ndizi
Kumgombaniza mvivu na usingizi
Yaani kucheka kwa furaha na mhalifu wako wakati wa fumanizi

Na inanichukua sekunde tu mi kukujua we ni nani
Maji ya kunde mweupe mweusi au kijani
Sio kila yaani kila mtu anamjua huyu chifu
Gusa unase kayupo kakupokelea pipu
Mwenye kisu ndo anakula nyama
Usiongelee bifu utachekesha
Kama sindano inayotetemekea jipu
Nimezaliwa nacheka ila simaanishi 
Mtakatifu ila ni mtu wa watu
MUNGU ndo ananilinda kila siku

Na sijui kama mnajua ila najuwa hamjui
Kwamba madogo wa siku hizi  wamekuwa hawakui
Watapanga sana safu kwangu dafu hawafui
Mbio ndefu hizi pub haya mapafu ni ya chui

Yaani boss najituma afu chenji sichukui
Navyowabana majanja mpaka hawapumui (Uuh! wiih! )
Bisha nikung'oe gego nikipiga  sichagui engo
Huwezi zuia msumari kwa kuvaa yebo

Weka dreams kwenye table ya vichwa panzi on fire 
Rapper wenu leo kwa roho nzuri nawafanya vibaya
Yani wakigusa waya hatari mashuti ya mbali wavu
Mistari ya uchi kama kuku aliyewekwa juu ya wavu

Na ukiongelea wakwanza una maanisha mimi
Speed kama Lamborghini nikiwa road ni moto chini pub
Ukiongelea washenzi na washenzi ndio sisi
Mbona una maswali mengi kwani we Police

Ukijichekesha si atucheki mood zetu hazieleweki
Tunaweza tukakulisha kinyesi na ulifikilia ni keki
Kwaiyo usibet maana maji yakimwagika hayazoleki 
Sio sheri siku hizi tunakutana Bank

Na haiwezekani bhana
Eti Yanga wafungwe me ni kazi
Na siku Simba wakitushinda mnikumbushe nihame 
Hapo game itakuwa over hata akija Zidane
Coz tunajua hadi ujuzi unaomba tujuwane

Me ni maji kwenye ukame Genius Cloud  ka Van Dame
Nipo dif na hakuna anayeweza force tufanane
Mtaka cha uvunguni hawezi puuza kuinama
Wakati wa amani ndo wa kujifunza kupambana

Alio nilazimisha nilale ndo alofanya niamke
Anayekupaka tope ukipata kitambaa unaamue ufute
Anayetaka usote ukipata chapaa unampa akumbuke
Anayetaka uwogope muonyeshe silaha
Halafu mwambie akuguse

Kazi kwenu wazee wa nguvu kontena akili kisoda
I'm the first and lonely ulinzi hata kwa jeshi la mtu mmoja
Young mwanza mwanza juu ya map  ya Dunia namba moja
Kwaiyo mtamwambia Roma arudi nyumbani kumenoga

Afu kuna jamaa me hapa amenipigia simu harafu simjui
Eti ananimbia why urafiki mwisho uadui
Nilimjibu sorry mambo ni moto me hata sijui
Kilichofanya hadi ngoma ya watoto ifike asubui

Eyooh Killer young waambie wanobana waachie
Siku wakiacha kunichekesha ndo watanifanya nilie
Mzee wa kunyoosha nanyoosha nawapa wanikunjie
Telephone free day ndo uwaambie wanipigie

Indiscipline jua imewaingia kichwani
Unasema unijui mimi we anayekujua nani?
Mmepanic naona mnachukia mpaka utani
Anayetaka kuwa mimi sasa  na mimi nitakuwa nani eeh!

Machungu yatabaki kwa watawaliwa
And we need life revolution meehn
Hey Greatest before to work up
I'm the first and lonely

Tunawarudisha darasani tupate mapinduzu ya akili
MUNGU anajua kila mtu atakuwa nani?
Ndo kwanza hauwezi kunitabili
Na lengo sio ku make trending
Jiamini kupata knowledge you can't know my brain
Hata ukisoma psychology
Mnaintroduce me of fomula street wananiiita
Haha eenh eh bwana..

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Sinaga Swagga 5 (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

YOUNG KILLER MSODOKI

Tanzania

Young Killer Msodoki  also known as Erick Kendrick is a rapper from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE