Home Search Countries Albums

Inatosha Lyrics


Kwangu ni sawa
Ata niwe kiziwi nisisikie lolote
Ila sauti yako tu
Kwangu ni sawa
Ata niwe na upofu nisione lolote
Nikuone wewe tu
Wala sitojali lolote
Sitoshika chochote
Kiu ya moyo wangu
Nishike neno lako tu
Ata nitengwe na dunia nzima
Wanifanye vibaya
Nikiwa nawe inatosha
Ata iweje, Nitalisifu jina lako
Maana unajua vile unanisemesha

Sauti yako ikiongea nami
Inatosha, Inatosha
Uwepo wako roho ndani yangu
Inatosha, Inatosha
Ulinzi wako ukinizunguka
Inatosha, Inatosha
Upendo wako unavyonipenda mimi
Inatosha, Inatosha

Pekee yako, Pekee yako
Pekee yako wewe
Pekee yako unatosha
Pekee yako, Pekee yako
Pekee yako wewe
Pekee yako unatosha

Bwana Mungu ukamuita Adamu
Uko wapi mwanangu
Mbona sikupati, Nakutafuta
Adamu naye akajibu
Niko huku nimejificha
Kwani niko uchi
Nimeogopa sauti yako
Nani amekuambia ya kwamba uko uchi
Kumbe Adamu kafungua sikio lake kwa adui
Nataka kusikia sauti yako tu
Sauti ya ukamilifu
Ambayo hapo mwanzo
Ilinifanya niwe kamili
Nataka kusikia sauti yako tu
Ambayo moyo wangu utajaa utoshelevu

Sauti yako ikiongea nami
Inatosha, Inatosha
Uwepo wako, Roho ndani yangu
Inatosha, Inatosha
Ulinzi wako ukinizunguka
Inatosha, Inatosha
Upendo wako
Unavyonipenda mimi
(Upendo wako kwangu)
Unanipenda upeo
Inatosha, Inatosha

Bwana
Pekee yako, Pekee yako
Unatosha
Pekee yako wewe
Pekee yako
Bwana, Unatosha
Pekee yako, Pekee yako
Pekee yako unatosha
Pekee yako
Pekee yako unatoshaa

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2022


Album : Inatosha (Single)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

WALTER CHILAMBO

Tanzania

WALTER CHILAMBO  is a Gospel Singer and Song Writer from Tanzania. He was the winner at Epic Bo ...

YOU MAY ALSO LIKE