Home Search Countries Albums

Wajinga Nyinyi (Part 2)

TEARDROPS POET

Wajinga Nyinyi (Part 2) Lyrics


Shots fired! Wacha tupump sense kwa hawa mashort wire
Hatuogopi kuface the music 
Si ndio choir master wa hii choir, so usiwahi gwaya
Wacha niichukulie penye King aliachia

Kwa hii nchi yenye kuwa masikini ni hatia
Truth ni bado hatujawahi pata uhuru
Sorry kusema sio kila tourist hukuja Kenya
Kuona Diani ama Samburu
Wengine hukuja kuona Kibera na Mukuru
Zile white collar waliahidi bado ziko
But kwa shingo ya kunguru

The rich also cry but so far
Ni Sonko mmoja nimesikia akipiga nduru
Starehe tuko na Jaguar moja tu na ni kama hainanga ngata
But si huiona mara moja tu time ya election

Wamama wajawazito ndio wanakuwa first priority kupiga kura
But hao ndio wanadedi kwa maternity due to lack of facility
Ambia KANU hatuhitaji jogoo tumeupgradi si kama kuku ya grade
Madem wa campus wanadedi, RIP Sharon na RIP Mercy Keino
Apart from ule governor wa Migori kuna mwingine anatu owe bado
Cartoons zikianza kumake sense kuna vile hii nation ina  owe Gado

Tulipata new currency but change haiko bado
Ama Kenya iko blessed na corruption
Ju 10% huwa inaenda kwa kanisa
Na badala pastor kusema rudisha mahali umetoa
Anasema zidisha mahali imetoka

Sadaka ya prostitute na mwizi zikimix kwa kikapu
Pastor huwa hawamind nani ametoa ngapi wala imetoka wapi
Kanisa ziko na fence sababu wanaogopa watu wataiba imani
Ama wataiba hii money

Mapastor wenye wanataka magari ni kama wako juu ya maombitho
Mbona unataka harambee na si maombi though
Political rallies zimejaa 
Coz wengi ni wafuasi ama sababu wengi wako jobless
God of all creation iko kwa National Anthem
Kama wengine wetu tunaishi kama children of a loser God 
Wajinga nyinyi mnachoma nyama na makahaba
Na familia nyumbani wanakula ugali na jaba

Tulipigania independence ndio tunyakue mashamba zetu
Kwa wakoloni only kuja kuzilose kwa hawa ma land-grabber
Tumebaki tu na Holy Spirit hatutrust kamwana na baba
Vijana tuliinvent kugota ju tulikuwa hatutrust handshakes
Now that hiyo ngumi imeinuliwa kwa sky 
Washaanza kufeel the earthquake

A minute of silence, sirence
Politician akinyamaza ameshiba akiongea amenyimwa
Vitu za free haifai hoteli zina free wi-fi
Na si free food, uko online kwa hoteli
Unashare picha za watu wenye wana njaa
Badala ya kushare chakula mjinga wewe

Tuko na njaa mngetulea kwanza 
Sababu hatuwezi shiba na thoughts and prayer
Zile mbegu tulipanda kanisani tungepanda Turkana
Zingelisha wengine pengine
You see, nyuma ya noti ya soo mbili
Kuna watu wanaharvest cotton
Na bado nation inaimport mitumba

Wacha nianze nikiquote Patrice Lumumba
Tuko kwa nchi yenye wenye wako na power, hawana idea
Wenye wako na idea hawana power
You see, ningetaka kusugar-cot vitu basi
Ningeanza kufanya biashara ya kaimati
Serikali ikasema kwenye umeiba tumeshaform kamati
Shida ni hakuna mwenye hufikishwa Kamiti
But hatuachilii mpaka tufike tamati

Watoto hawana playing field na stadiums
Zenye ziko, ziko kwa manifesto
The next kipchoge anakimbilia kwa trademill probably
We’ve been in the dark for too long
Token za KPLC zikuje kama essay
After three days ndio upate the light tuko sawa
Wakulima waliuproot miti za kahawa wakapanda mahogany
Ndio atleast wakidedi na njaa 
Wakuwe wamebenefit macoffin maker na sio macoffee maker

Ulisema security begins with you, NO
Security doesn’t begin with you it begins with S
What begins with U ni ufisadi, ubinafsi, ukabila
Uwizi wa mali ya umma, upuzi, ujinga, uporaji, uongo

If you are what you eat then how comes sijawahi
Come across polisi anaitwa mlungula ama hongo
Ni accident ama ni traffic police
Ndio hukufanya we kufunga mshipi
Mi deni yangu yote ilishapoa on the cross
So hiyo ya China mi silipi
Barabara zikiwa na mashimo complains
Zinakuja na watu wako na gari personal

Mtoto akienda shule nursery imejaa mashimo
Inakuwa ni issue ya mzazi personal
Si mtoto alisare shule 
Sababu hakuwa anaweza afford sare ya shule
Akaamua kuwa mwizi alafu mnasema ni sababu ye kutoenda shule
Mkaamua kumrudisha shule when its too late
Mkiexpect akuwe measy shule akaend up kuwa mwizi yule

Simba si Baboon usiexpect kuirushia ndizi ikule
Si kila mwaka unapewa lesso kwani hujawahi pewa lesson
It seems like a common sense ilienda vacation
Mlishatuvunja miguu, alafu mnaexpect standing ovation
You see, kwetu kwa ground vitu si different
Kwa ground si humake the difference
Si mnaweza kill the King but not the prophesy

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2019


Album : Wajinga Nyinyi (Part 2) (Single)


Copyright : (c) 2019


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

TEARDROPS POET

Kenya

Teardrops Poet real name Mark Joshua Ouma is an artist/Poet from Kenya.  ...

YOU MAY ALSO LIKE