Home Search Countries Albums

Sanitize Lyrics


Nilikuwa sapa na Uhunye, lunch na Ruto
Na mpaka wa leo nashangaa mbona sijawai jo shiba
Infact siku hizi ndo nakunywa zaidi
Mpaka mathangu anachocha mtoi wangu ni kaa siku hizi anaishi bar

We chorea tuliacha kuvuta zile za Zanzibar
Btw sai niko married niliacha kutoa mamanzi bar
Imagine mtoi alikosa sare juu budake alimadwa bure
Mi the only time am looking for Caro 
Ni saa zile nataftia Azam doh za shule

Mtaa hakuna security unaweza shikwa na maboy
Gava na but hatujali ju hata Nairobery yetu sai 
Tunaishi bila jo governor
Bro kuna vitu zinanibamba na kuna zingine hazinibambi 
But to hell atleast sai kuna virusi zinashika hadi mababi
Mbona mtaa mtu wangu hakunaga maji safi?
Na vile mtaa naskianga inaekwa iwe maji ya Wasafi

Mbona waheshimiwa ni walafi hadi Kilifi
Wanajichocha na bursary si tunatafuta mtu anweza kill hii fee
So saa zile wanajisanitize mikono
Si tunajisanitize akili na akili si mwili

Hii ndio life mama mboga kwa soko
Mume ako home analia ako msoto
Hakuna hustle ya kutaftia watoto
Ju gava yetu imejaa tu wanoko

Sanitizer ni thao, kibeti na mbao
Nashindwa ni how, tuwaulize how
Tunaishi kama ng'ombe si hatuna makao
Hatuna makao (Kao)

Ninachumia kwa jua mpaka inapotua
Naraukia kuomba dua Mungu ataniepua
Jana, leo shida kila tour
Nalia navumilia ila najitambua

Mwaka unaanza tu na visanga vikifuatanaga
Mpaka zinafanya tunashtukaga tunaogopa kuaga
Mara locust kwa mabroadcast zinatanga tanga
Sai Corona imakuja kutuongezea matanga

Stress ni nyingi vijana wanategemea mashada
Tunahepa jiji kwenda ocha tukalime mashamba
Hakuna wera wengine wanalala kwa vibanda
Na ukijibonda huku nje unaweza kulishangwa pamba

Lakini bado hatuchoki kupambana
Ju hii ni Kenya na tulishazoea drama
Chinjeni dume msinichinje mi ni ndama
Ata ikizidi maandamano tutafanya

Hii ndio life mama mboga kwa soko
Mume ako home analia ako msoto
Hakuna hustle ya kutaftia watoto
Ju gava yetu imejaa tu wanoko

Sanitizer ni thao, kibeti na mbao
Nashindwa ni how, tuwaulize how
Tunaishi kama ng'ombe si hatuna makao
Hatuna makao (Kao)

Hii ni ya kila mtu mwenye jina yake haiko kwa google
But ye huamka kwenda ku-search
Hii ni ya kila fundi wa viatu mwenye hurauka kazini
Akijua kuna soles kadhaa anafaa kutouch
From ule kijana anatrek akienda Industrial Area
To yule mama mwenye anakimbia Clinic na newborn
Coz ako na symptoms za Malaria

From wale wenye wanaenda mjengo wakiwa wamedandia lorry
Na hawako sorry about their story
To wale hawawezi tembea juu miguu imejaa na jiggers
Our problems might be big but our God is bigger
From yule graduate mwenye ako na PhD 
Na anafanya kazi kama conductor
Hoping one day that ataleta change

Si wote hatuna difference na dentist
Sababu tunaishi on hand to mouth
Si huwa tunategemea Mola
Maisha ni safari na ni kama 
Wengi wetu tulikula fare
Maisha ni safari 
Tunahope one day itakuwa barabara

Hii ndio life mama mboga kwa soko
Mume ako home analia ako msoto
Hakuna hustle ya kutaftia watoto
Ju gava yetu imejaa tu wanoko

Sanitizer ni thao, kibeti na mbao
Nashindwa ni how, tuwaulize how
Tunaishi kama ng'ombe si hatuna makao
Hatuna makao (Kao)

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Sanitize (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

SSARU

Kenya

Sylvia Ssaru (born on 19th May 2002) aka 'Saru wa Manyaru' is s a Singer, Song writer, ...

YOU MAY ALSO LIKE