Home Search Countries Albums

Sifa

ROSTAM Feat. BEN POL

Sifa Lyrics


It's Rostam baby
Eeh eeyaaa...
(Wamemchokoza bear)

Umepewa nywele sasa weaving wigi la nini?
Nitashindwa mimio hii ligi ya umasikini
Nyoa hata para upunguze hela ya mafuta
Au punk ka chotara kinyakiusa mamushka

Nayo macho ulipewa unione mimi tu 
Kitu ambacho am so proud of you
Amini kwamba sitoruhusu yamwage machozi 
Kama namba we ni tisa mimi ni sita
Yes of course and am pretty sure
Kama msomali hiyo pua
Ingejengwa na tofali ingeendeleea kuyafyatua

Mungu ni fundi na nusu kakupa mashavu soft
Ya kupiga mabusu sio kupiga makofi 
Na ilo sikio ulopewa usilitoboe toboe bibie
Mwisho utaitoboa ngoma hadi mumeo usinisikie
Na hayo meno yasining'ate mdomo ninyonye nidate
Ulimi ulambe aste aste na moyo wako unifwate

Nifanye kama niko peke yangu dunia nzima
Usinifanye kama your ex boyfriend
Uko mikono salama kwenda kwa wazazi lazima
Nakupa vyeo makuruta wanyooke

Sifa zote unazo
Kichwani mpaka unyayo 
Umepewa utajiri
Wa urembo wa siri 

Tumia, tumia 
Tumia, tumia mama
Tumia, tumia 
Tumia, tumia  eeh

Hio shingo ulopewa sio ya kuvalia mikufu
Ni vyema ukavaa Tas B ama rosary tukufu
Please usipende kuhonga mikono mashoga
Maana hio mikono umepewa kuungia mboga

Kifuani chuchu dede mpaka sijui ni saa ngapi
Mama umepewa maziwa watoto wavulie samaki
Umepewa tumbo hili tujaze dunia
Sio la kulia kiepe nyama choma wala bia

Kuna sehemu umepewa sio lazima kuitaja
Mungu Bwana kaificha katikati ya mapaja
Mi mwafrika watu weupe nawachukiaga
So nikibeba wazungu naonaga bora kuwamwaga

Hicho kiuno ulichopewa sio cha kuchezea baikoko
Bali tukiwa chumbani uno feni fifi moto
Hutopewa paja na mguu uvae vikuku na vimini
Maana utanipa taabu ya kupambana na wanaopenda chini

Sifa zote unazo
Kichwani mpaka unyayo 
Umepewa utajiri
Wa urembo wa siri 

Tumia, tumia 
Tumia, tumia mama
Tumia, tumia 
Tumia, tumia eeh

Sauti hio ya kuniita
Mwendo huo wa kunifuata
Kucha hizo za kunishika mama
Tujenge ngome nawe isivunjike kamwe
Pamoja mi na wewe, yeah

Sifa zote unazo
Kichwani mpaka unyayo 
Umepewa utajiri
Wa urembo wa siri 

Tumia, tumia 
Tumia, tumia mama
Tumia, tumia 
Tumia, tumia eeh

 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Sifa (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ROSTAM

Tanzania

ROSTAM  is a music group made up of two tanzanian rappers ROMa and Stamina. ...

YOU MAY ALSO LIKE