Home Search Countries Albums
Read en Translation

Kwetu Lyrics


Sifa kwa Mola wangu Maulana kwa mengi aliofanya
Hadi mi na we kukutana kisura
Sijapanga kudanganya ntasema ukweli mama
Kisa nakupenda sana kisura
Umesema wanipenda ila maisha yangu maseke
Michicha milenda ndo menyu yangu na ya kuku mateke
Yaani chenga kila siku kilio sa lini nicheke
Sina tenda ugali Buguruni mboga Temeke
Nafurahi umeniridhia niwe na wewe kimwali
Maisha yangu mitihani isoisha maswali
Ukifika nyumbani vumilia maana hali sio swali
Asubuhi mchana pakavu jioni ndo kula futali
Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee suala la nyumba na gari mimi
Bado mi bado mi bado
Ndo kwanza nimepanga
Bado iyee mi bado
Sina hata kiwanja
Bado iyee mi bado
Kulipa kodi majanga
Bado mimi bado mi bado
Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro
Ghetto namkeka tu hakuna kitanda shuka wala godoro
Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya Comoro
Ila nimeshakupa nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa utanizika mzima mzima
Nimeshakupa eh nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa ah utanizika mzima mzima
Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee suala la nyumba na gari mimi
Bado mi bado mi bado
Ndo kwanza nimepanga
Bado iyee mi bado
Sina hata kiwanja
Bado mie mi bado
Kulipa kodi majanga
Bado mimi bado mi bado
Suala la nyumba na gari mimi
Bado mi bado mi bado
Haki ya Mungu bado yaani shuka bado
Ndo kwanza nimepanga
Bado iyee mi bado
Sina hata kiwanja
Bado iyee mi bado
Kulipa kodi majanga
Bado mimi bado mi bado

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2016


Album : Kwetu (Single)


Copyright : ©2016


Added By : Trendy Sushi

SEE ALSO

AUTHOR

RAYVANNY

Tanzania

Raymond Shaban Mwakyusa (born 22 August 1993), better known by his stage name Rayvanny, is a Tanzani ...

YOU MAY ALSO LIKE