Home Search Countries Albums

See You Lyrics


(Dear mama I see you mum)

[VERSE 1]
Aaah yeah
Kifo hakikuangalii uwe rais au mmbunge
Na pia hakibagui mwembamba wala kibonge
Hakikuangalii tajiri au maskini
Na pia hakichagui mpagani ama una dini
Kweli kifo nimeamini
Hakina huruma, kinajua siwezi
Kikamchukua baba na mama
Kimefanya niwe na simanzi
Machozi mengi usoni
Kupoteza wazazi na kukosa furaha duniani

Hivi kifo kwa nini katili sana
Haubagui rika wazee mpaka vijana
Kama Utani the great ukamchukua Wasara
Umempa simanzi sir Juke ulipofatia kweli
Kila nafsi lazima ionje mauti
Wapo wanazikwa na sanda wengine huzikwa na suti
Unapofika mtu anashindwa kuongea
Kweli kifo ni katili umemchukua mpaka Ngwea?

[REFRAIN]
I'll see you if you get there
If you ever get there
See you when you get there
I'll see you if you get there (dear mama)
If you ever get there
See you when you get there

[VERSE 2]
Haijalishi unafanya nini duniani
Kifo kinadharau kejeli wala utani
Utakufa vipi jiulize au vitani
Au umelala usingizi kwa kitanzi shingoni
Ukitenda mema lazima uende peponi
Ila ukitenda dhambi lazima uende motoni
Sometimes unashindwa kusonga mbele
Mwanzo umetupa pigo kwenye MV nyerere

Umechukua watoto, mama mpaka mababu
Akili zetu kwa kweli unazipa taabu
Upo conscious wala hutaki vicheko
Tasnia umeipa pengo kumchukua King Majuto
Remmy alisema nawe lakini wala haukumjali
Ulivyo katili ukamfyekelea mbali
Hautaki vituko wala madrama
Maskini ukamchukua oooh mama

[CHORUS]
I'll see you if you get there
If you ever get there
See you when you get there
I'll see you if you get there (dear mama)
If  you ever get there
See you when you get there

[VERSE 3]
Nawaza lakini jibu sijapata
Najua ipo siku nami pumzi yangu nami itakata
Na pia sitapata ata nguvu ya mic kushika
Wanangu wabugurika tabaka lasikitika
Hauhitaji washikaji wala wapambe
Haukuogopa shepu na sura ya Masogange
Ukija kwangu niambie ili nijipange
Ikibidi nipe kodi, sio ghafla kama kinyambe

Hauogopi kila kona we unachimba
Sasa umeliacha pengo baada ya kumchukua Madiba
Unahuzunisha tarafa mpaka taifa
Tisa tisa umetuliza kumchukua Baba Taifa
Unajiamini sehemu zote wewe unatamba
Stejini ukamchukua Papa Wemba akiwa anaimba
Haujali ata watu wanaopendana
Complex na Vivian ungewaacha si wangeoana?

[CHORUS]
I'll see you if you get there
If  you ever get there
See you when you get there
I'll see you if you get there (dear mama)
If  you ever get there
See you when you get there

 

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2018


Album : See You (Single)


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

NCHAMA THE BEST

Tanzania

MCHAMA THE BEST is a rapper and songwriter frm Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE