Kidani Lyrics
Kidani changu unang'aa
Kidani changu cha thamani
Wewe ni muhimu maishani
Unang'aa sana kwangu moyoni
Nakuomba uwe nami milele duniani
Naomba utambe vile vile jisifie
Usijali we jigambe wenye chuki waumie
Nataka nikuvae daima shingoni mwangu
Na vile vile ung'ae daima moyoni mwangu
Nataka leo niimbe ili dunia ijue
Na daima nikubebe Yani kamwe nisikutuee
Kidani kidani kidani
Kidani unang'aa
Usiogope maneno yanayosemwa na watu
Maneno ni herufi zilizopewa sauti
Na vile vile jichunge na chuki za majirani
Waambie kuwa Mimi nimekuweka moyoni
Kusema ukweli kidani changu unaniliwaza
Mimi nakesha kichwani mwangu kutwa kukuwaza
Nataka nikufiche mbali wasikuone
Nikuepushe na ajali na daima uzidi kung'aa
Unang'aa zaidi ya dhahabu na almasi
Kukutunza inabidi na hii ndio sababu
Kidani kidani cha thamani
Kidani kidani kidani cha thamani
Kidani unang'aa
kidani unang'aa
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2023
Album : Kidani (Single)
Added By : Derick Buliro
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE