Pumzi Lyrics

Chozi lanishuka najiponza kwa mvinyo
Mahaba nishasusa huko mimi simo
Maana hai ulishanizika
Kanichimbia na shimo
Nikate pumzi nitoke duniani
Mautam na utam, mautam ya hamu
Ila mwisho ni uadui na sijui
Hebu niambie mmmh
Tulivyopanga ikasanda nitulie
Ukatanga na kudanga, niambie mama
Penginee (penginee)
Ntulie bwana na uadui
Hukushiba na makopa wewe
Japo vingi vyanichocha mi nilewe
Ukionywa unafoka ila wewe
Yako kali sumu nyoka
Maanake mimi nilikupenda wewe zaidi
Sikuwahi hata kucheat niliyoyatenda Mungu shahidi
Tunda nimelipopoa mwenyewe shamba la bibi
Wajanja wakanizidi kukuacha sikutaka ila imenibidi
Fahamu kuwa siwezi kula wali mkavu mgaagaa na upwa
Mwili umenikongoroka imebaki mifupa
Taja ulichokitamani nkakataa kukupa
Uko kwa wahuni utatumika sana ukichakaa unatupwa
Nikaona tu nikubwagie manyanga
Kipi cha kung'ang'ania pisi yenyewe majanga
Nikienda kazini ghetto unaniletea waganga
Ili nisiwe na neno akiniaga kuelekea kudanha
Vingi nilikupa funguo za mkoko
Vinguo vya mtoko kila wiki vizawadi
Mahaba motomoto
Ukipika napenda hata ukitoa bokoboko
Ila kwa kuwa dawa ya moto ni moto
Utazimwa na moto wa msoto
Hebu niambie mmmh
Tulivyopanga ikasanda nitulie
Ukatanga na kudanga, niambie mama
Penginee (penginee)
Ntulie bwana na uadui
Hukushiba na makopa wewe
Japo vingi vyanichocha mi nilewe
Ukionywa unafoka ila wewe
Yako kali sumu nyoka
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Pumzi (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE