Home Search Countries Albums

Vimba Lyrics


Wahenga walisema 
Penzi lamea penye penzi
Twendelee kupendana
Japo wapo wanaoumia

Sasa naiona
Sasa naiona dhamani ya mapenzi
Kwako mimi
Kwako nimedidimia

Vile tu tulienzi
Hata kwa ugali na bamia
Tubembelezane kwa tamu tenzi
Hata tunapoikosa mia

Vimba mpenzi(Vimba)
Jidai mpenzi(Vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaaaa...vimba

Vimba mpenzi wangu eeh(Vimba)
Jidai beiby wangu eeh(Vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaaaa...vimba

Pua pua wanaokejeli
Chaguo langu mama mama
Ukitazama kuwaliko wao ni vituko

Furaha, 
Furaha imetambaa kwangu
Wao kila siku 
Msukosuko

Wanajijaza masusu
Na mambo yasowahusu
Tusipuuze zao figisu
Vikwazo tusiruhusu

Vimba mpenzi(Vimba)
Jidai mpenzi(Vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaaaa...vimba

Vimba mpenzi wangu eeh(Vimba)
Jidai beiby wangu eeh(Vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaaaa...vimba

Tupendane kwa hali na mali mama
Tusiwe kama manenge na mandawa
Eeeh maadui wapambane na zao hali
Sie malavidavi, malavidavi mama aah

Ah subira huleta kilicho mbali
Kipendacho moyo ni dawa

Eeh mwaiona eeh(Mwaiona)
Bendera yetu yapepea(Mwaiona)
Safari yetu yaendelea(Mwaiona)
Chuki zao twazipotezea(Mwaiona)

Vimba mpenzi(Vimba)
Jidai mpenzi(Vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaaaa...vimba

Vimba mpenzi wangu eeh(Vimba)
Jidai beiby wangu eeh(Vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaaaa...vimba

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2019


Album : Vimba (Single)


Copyright : (c) 2019


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ISHA MASHAUZI

Tanzania

Isha Mashauzi aka 'Queen of melodies' is an artist/vocalist who sings and performs Taarab mu ...

YOU MAY ALSO LIKE