Nisaidie Lyrics
Mateso yakizidi, hofu hutawala
Hakuna tumaini, lini yatakwisha?
Imani yatoweka, hakuna tumaini
Mungu wangu nisaidie
Hakuna hata mmoja aniwazie mema
Adui wamezidi rafiki wageuka
Sioni hata mmoja wa kunisaidia
Baba wewe, Mungu wangu nisaidie
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda
Nguvu zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Nakungoja wewe nipe nguvu mpya
Nipeperuke kama tai nitembee bila choka
Nipige mbio mbele bila kuzimia
Mungu wangu nisaidie
Nimeshajinyonyoa manyoya
Nimeparua kucha kwa amani
Nimepunguza uzito wa mwili
Niko tayari kuruka tena
Maisha yangu ya pili mazuri
Kulinganisha na yale ya kwanza
Niko tayari ninazo nguvu
Kama tai
Ujana wangu umerejea
Maisha yangu yamerejea
Sasa niko na nguvu
Sionewi tena
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda
Nguvu zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Nisaidie,nisaidie
Nisaidie, nisaidie
Wale wamngojao Bwana
Watapata nguvu mpya
Watapaa juu kwa mbali
Kama tai oooh
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda
Nguvu zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Mungu wangu nisaidie
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda
Nguvu zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Mungu wangu nisaidie
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2019
Album : Nisaidie (Single)
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
FRED MSUNGU
Tanzania
Fred Msungu is a pastor , author and the founder of Pure mission (Tanzania ) Other aspects of Fred ...
YOU MAY ALSO LIKE