Home Search Countries Albums

Nchi ya Kitu Kidogo

ERIC WAINAINA Feat. REDYKYULASS

Nchi ya Kitu Kidogo Lyrics


Mzee alisema hakuna cha bure
Huo msema tumeutafsiri kinyume
Hata shule kuiingiza mtoto
Lazima utoe mchoto
Kupata simu ni balaa
Road license bei nafuu utanunua
Kupoteza ID ni mashaka
Twaarudisha Jamhuri yetu nyuma

Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu 
Nenda Limuru (Nenda Limuru)

Hata nyumbani ukipatwa na majambazi
Kupiga 999 wasema "Sisi hatuna gari"
Lete elfu tano ya petroli, saidia utumishi’
Mahakamani hela ndio haki
Kwa elfu chache mshtakiwa ndiwe mshtaki
Utajiri huwa ushahidi
Twarudisha Jamhuri yetu nyuma jamani

Nchi ya kitu kidogo
ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka soda ewe Inspekta burudika na Fanta
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe Mama nunua Ketepa

Huko Kenyatta madawa zimeisha
Mashiti zauzwa marikiti mia kwa mia ah
Wafanyi kazi waenda miezi bila pesa
Ni bahati ukitibiwa

Mzigo wetu nazidi kuwa mzito
Watoto wanne na mshahara wa elfu mbili mia tano
Ya viatu, ya vitabu na vyakula
Nauliza na Mbotela ‘Je, huu ni ungwana?’

Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu nenda Limuru

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Nchi ya Kitu Kidogo (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ERIC WAINAINA

Kenya

Eric Wainaina is an artist from Kenya. He is best known for his partriotic songs for Kenyans. ...

YOU MAY ALSO LIKE