Home Search Countries Albums

Money Lyrics


Money makes the world go round
Money makes the world go round
I say money makes the world go round
Money makes the world go round
I heard makes the world go round
Money makes th

Ikasikika sauti wananchi tuna msoto na mashaka
Pesa imefichwa  na kigogo mwenye madaraka
Mjira hamna maisha hovyo tumechoka kusafa
na kuanzia sasa tunaingia chocho kwenda kukaba
Akapita kibopa mwenye afya
Akiwa ana suti kali ni dhahiri ametoka kwenye Hafla
Hakusalimia kwakuwa ana kiburi
Ila ghafla akajikuta kwenye kona la kibaka
Kona la kibaka asiyezubaa hasira imemjaa
Amechakaa life imemchapa
Kamvaa kibopa kampiga roba matata
Pochi ikadondoka muhuni akaokota akachapa raba
Masaa kama nane kibaka hajala hata
tumbo linadai na isitoshe jana alilala kapa
Akaenda kwa mama Muuza akapiga Nguna
Alafu kabla hajasepa akauliza "nikilala huduma nitapata?"
Muuza ni dada fulani mwenye bodi tata
Kipato hakimtoshi anahitaji kodi ya alipopanga
Mwenye nyumba ni mgomvi anahoji anataka mkwanja
Anasomesha mtoto Boarding ana boarding wanataka ada
Mtoto anayelipiwa ada ye hayuko shule
Shule amechoka anatoroka anauza ngada
Tatizo lake mzembe alipewa mzigo akaupoteza
Na anadaiwa na bosi mtata
Sasa ameshahamaki yuko njiapanda
Mkono mmoja kwenye kichwa mwingine ameshika ada
Anataka kumpa Mtasha anawaza hela haitoshi anaahirisha
Anaenda kwa Pusha kuvuta ganja

Money makes the world go round
Money makes the world go round
I say money makes the world go round
Money makes the world go round
I heard makes the world go round
Money makes the world go round
Money makes the world go round
Money makes th

Anafika kwa Pusha anapewa
Kipuli anavuta mastimu anapata
Anatoa mpunga ili amlipe pusha
Pusha hajainuka mzuka umepanda
Pusha kaona Polisi wakuda kama saba
Pusha hajaficha Puya anakuta mbwa wametanda
Dogo kaangusha mpunga kasepa Pusha kasanda
Hawezi furukuta kuruka ukuta kote wamesanda
Riziki mafungu saba wanasema
Pusha kafunua yote mafungu saba hajapata hata moja
Polisi wanaona Pusha hana ujanja
Ni aidha waelewane au aende Central akanyee makasha
Pusha akaokota mpunga ule mpunga dogo kauacha
Akihesabu ni nyingi na bado anatoka kapa
Akawaza akimbie labda akaogopa maana
Mmoja ameshika Maga kubwa SMG chata
Akampa mkuu chake na wale wenzake akawapa
Kila mmoja akala zake akaenda zake kudampa
Mmoja gambe mwingine anajua kwamba
Anahitaji dawa kwa maana mkewe anaugua Kansa
Mwingine ni kamali amekubuhu hawezi acha
Kufika kwa Sadali kazungukwa na Mashanta
Na habari wote tayari wanaijua namba
Yaani hata ucheze kwa shari mali hauwezi pata
Kila akicheza hola anaokota garasa
Akicheki mkwanja unatoka anaanza kuogopa karata
Chombo kinaenda mrama, mchuzi  umekosa radha
Pesa sabuni jamani Polisi akaanza kudata, Coz

Money makes the world go round
Money makes the world go round
I approve that Money makes the world go round
Money makes the world go round
Money makes the world go round

Ikasikika toba tena kwa sauti ya kwanza
Wajanja Mkwanja wamekomba na mjinga nauli imekata
Maniga wamekomba dola wamezama machaka
na Wasaa wa kugawana chapaa ndio ikawa utata
Akasikika dogo " Nawaheshimu sana mabradha "
Mnafanya mgao gani ambao siuhafiki hasa
Vile mimi ni mdogo mnanifanyia undava
Hamuwezi mkagawa kote alafu mimi Mkaniacha
Mshata akajibu akasema dogo kausha kwanza
Hauwezi ukapaza sauti mahala ambapo hauna chata
Hauna ubavu hauna title kauli hauna Kaka
Hauna mo
Dogo akakunja ndita hasira kushinda Mdada
Aliyepima akajikuta na Mimba baada ya kubakwa
Gadhabu ya kwanza ishu kuwaza
Akakata shauri akachukua kisu akaanza kumfata yule kaka
Sauti ya uchungu ikasikika dogo aking'aka
Nipeni haki yangu la si hivyo moto utawaka
Mkononi zana kali akamfata braza
Uku braza anatamba kama ubavu anza kunikata
Tumekulea sisi hapa mjini kabla
Haujaanza kujua jiji kipindi kaka yako kafa
Alileta ujuaji mwingi kama ufanyavyo wewe
Tukamchinja mwili Kibiti kichwa Msata
Aliishia hapo hakumaliza hata
alichotaka kuongea alitoa macho kama kakabwa
Maneno hayatoki tena hali ime-change ghafla
Kisu tumboni kauli imekata ndio maana wanasema kuwa

Money makes the world go round
Money makes the world go round

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2023


Album : The Verteller (Album)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

DIZASTA VINA

Tanzania

Dizasta Vina  (real name Edger Vicent) aka "The Black Maradona" is  Hip-hop arti ...

YOU MAY ALSO LIKE