Home Search Countries Albums

Nimekoma Lyrics


Yalivyonifanyia mapenzi 
Mi siibi yangu tu
Oooh kila siku mimi wa kuyasujudu

Sitaki kurudia hiyo hali 
Bachela wa nguvu
Naapa yamini mpaka aamue Mungu

Yamechubua nafsi yangu 
Vipi nidanganye
Nizame kila siku 
Kwenye mapenzi nikwame
Kuparamia paramia

Mwenzenu naomba nikome 
Mapenzi rungu mwiba
Nikikupata sumu halina tiba
Mwenzenu nimekoma 

Kupaparukia haja zangu
Ila leo nimekoma
Yakafanya nikaonekana ngoma
Mwenzenu nimekoma

Na japo yana matamanio 
Macho yangu ila nimekoma
Na mapenzi ya leo ooh

Huwezi amini kuwa 
Nilidanganywa niko peke yangu
Lisilo ubani lenye kuvunda
Likavunda penzi langu

Ya nini ujipe taabu?
Mapenzi hayana ustaraabu
Wengi wameyapa adhabu
Wenye mali na makapu

Maumivu pia, sawa
Wenye uaminifu kiza haya
Nini cha kuuliza Bwana?
Tafuta size yako maana

Boresha boresha, sawa
Nitakukomesha, haya
Na kwanini unakesha, haya
Machozi yanatoka

Naamua mwenzenu nime-koma
Kupaparukia haja zangu ila leo nimekoma
Yakafanya nikaonekana ngoma mwenzenu nimekoma
Na japo yana matamanio macho yangu ila nimekoma
Na mapenzi ya leo ooh

Na si mi nakimbi kimbi kimbi kimbia (Mbio)
Mapenzi nayakimbia (Mbio)
Sipaki kurupukia, leo nimekoma

Oooh nakimbi kimbi kimbi kimbia (Mbio)
Mapenzi nayakimbia (Mbio)
Oooh nimekoma

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Nimekoma (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

BARAKAH THE PRINCE

Tanzania

Baraka Andrew Odiero better known as Barakah the Prince, is a singer and songwriter from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE