Home Search Countries Albums

Kiatu Kivue Lyrics


Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue
Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue
Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia
Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue

Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu
Nataka ninene nawe, nataka nikutumie
Nataka nikuinue, nataka nikubariki
Watu wangu waangamia, taifa langu la Israeli
Watu wangu wanasononeka, watu wangu wanateseka
Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we

Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we
Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia
Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu
Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu

Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu
Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu
Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu
Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia

Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we
Kitakupekea jehanamu hicho kiatu
Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu
Nataka ninene nawe, maana ninakupenda

Nataka ninene nawe, ili nikuokoe
Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee
Mimi sitaki uangamie, maana mimi ninakujali
Mimi Mungu ni wa neema, mimi mungu ni wa upendo

Ukitaka Mungu akubariki lazima kiatu kivue
Ukitaka kuinuliwa wewe ni lazima kivue
Wivu ulio nao wewe ni lazima kivue
Hutaki kuona mwenzako mama akiinuliwa wewe

Hutaki kuona mwenzako akiwa amependeza
Hutaki kuona mwenzako akiwa yuko smart
Tabia ulio nayo mama ninakwambia wewe
Hutaki kuona ndoa ya mwenzako jamani mke na mume wakicheka

Tabia uliyo nayo baba, nakwambia badilika
Hutaki kuona huduma ya mwenzako jamani likisonga mbele
Hebu kivue, jamani hebu kivue
Kiatu cha nyumba ndogo, kiatu cha ulevi
Kiatu cha uzinzi, kiatu cha masengenyo
Kivue, kivue, kivue,

Mungu ananena nawe hicho kiatu kivue
Mungu anena nawe hicho kiatu kivue
Valia mini waume wa wenzio iwe mwisho
Kuvalia vitovu waume wa wenzio iwe mwisho

Kupaka wanja kwa waume wa wenzio iwe mwisho
Nataka nikupe mumueo, nataka nikupe nyumba yako
Nataka nikuinue, nataka nikuinue
Nataka nikuinue, niinue mume wako

Niinue nyumba yako, nimwunue mke wako
Nikupatia mchumba, kiatu cha nyumba ndogo
Mungu anasema nawewe hicho kiatu kivue
Kivue, kivue, kivue, kivue
Ah, hicho kiatu kivue

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2011


Album : Kiatu Kivue (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ANNASTACIA MUKABWA

Kenya

Annastacia Mukabwa is a gospel artist from Kenya. ...

YOU MAY ALSO LIKE