Home Search Countries Albums

Wapo (Cover)

ANAYA

Wapo (Cover) Lyrics


Hivi kwanini nijitutumue
Na dunia sio makazi
Vijineno neno vinisumbue
Hadi nishindwe kufanya kazi

Mama alisema mkuku kwa nguruwe
Kuishi na watu kazi
Achambe atukane ata aniue
Nishasamehe mzazi ni mzazi

Mwenzenu naficha naficha
Mengi ninayoyaona
Kifupi nafunika kombe
Nikiamini kesho nayo siku

Mapicha picha mapicha
Sidhani kama nitapona
Wanangu wa mtaani mniombee
Hii vita ni mchana na usiku

Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao

Oooh ni kama watu
Kumbe ndani wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao

Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi

Uniamshe alfajiri
Kama jana na juzi
Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu Baba mwamuzi

Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wasotaka ufanikiwe

Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema
Nah nah nah nah mmmh

Watakuita mwanga kibonge
Tena kwa dharau wakucheke
Wanachotaka waongee
Waseme shukrani ya punda mateke

Kama vipi dem wake tumgongee
Ndo anayempiga chura teke
Usipoonewa ndonge
Basi ndo ujue hauna makeke

Sikia Konde we pambana mjini shule
Ukipata kidogo letana nao tule
Wachana nao wamesemaga umezoea vya bure
Maana siku zote nyani halioni kundule

Kama baba na mama ndo nguzo ya dunia
Wapende wote
Sio wa kike anacheka wa kiume analialia
Bila msaada wowote

Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao

Oooh ni kama watu
Wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao

Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi

Uniamshe alfajiri
Kama jana na juzi
Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu baba mwamuzi

Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wasotaka ufanikiwe eeh

Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Wapo (Cover) (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

ANAYA

Tanzania

Anaya is an artist from Tanzania. ...

YOU MAY ALSO LIKE