Jivunie Chako Lyrics
Ndoa ni kkwanza kuelewana (sio fujo, mateke na ngumi)
Ndoa ni kkwanza kuelewana (sio uwanja wa mapambano)
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, fuhara ya moyo wako
Nawahasa msigoùbane tena
Na ndoa yenu msilie tena, uliyempata leo ndiye kipenzi chako
Siunajua mmekubaliana
Kweli ni kwamba nyie mnapendana
Ndio maana tumekuja leo
Tumalize jambo lenu
Hivi unajua ilikuwaje
Mpaka huyo eva apatikane
Huyo eva alitoka kwenye ubavu
Ubavu wa mwanaume
Adamu kasema sasa huyu mifupa katika mifupa yangu
Na nyama katika nyama yangu
Ataitwa mwanamke
Kwa hiyo sasa huyo mwanaume, atamuacha baba yake
Atamuacha baba yake na mama yake tena
Aambatane na mkewe, wakaishi kwa fuhara
Watakuwa mwili mmoja wataishi pamoja
Hivi unajua ilikuwaje huyu bi harusi apatikane
Bwana harusi hatika amepambana ampate kipenzi chake
Twawaombea mkafurahi vicheko utani na raha nyingi
Watu wote leo tuko hapa tumalize jambo lenu
Ndoa ni kwanza kuelewana (sio fujo, mateke na ngumi)
Ndoa ni kkwanza kuelewana (sio uwanja wa mapambano)
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, fuhara ya moyo wako
Watu wamekuja kuwapa mji ndugu na rafiki
Wote wamefurahi kuwa hapa kwa ajili yenu
Basi sasa msipigane mpendane mchukuliane mbebane
Mvumiliane muwe wakufichiana siri
Ugomvi na hasira hasira msifanye mueleweshane kwa upole
Majibu mazuri upalilia upendo
Na kwa sasa sisi tumeridhika taratibu zote mmezifata
Kama vile bwana mungu aliagiza, mfunge ndoa takatifu
Kikubwa sasa twawaombea mungu awape maisha marefu
Yenye baraka furaha pia upendo katika nyumba yenu
Basi sasa msipigane mpendane, mchukuliane mbebane
Mvumiliane muwe wakufichiana siri
Ugomvi na hasira hasira msifanye mueleweshane kwa upole
Majibu mazuri upalilia upendo
Usimpige mkeo utakuwa wajipiga mwenyewe
Maana sasa nyinyi ni mwili mmoja
Utajiumiza mwenyewe asipoumia mwili atakua ameumia moyo
Nawe pia utajiumiza moyo, furaha ukosekana
Ndoa ni kwanza kuelewana (sio fujo, mateke na ngumi)
Ndoa ni kkwanza kuelewana (sio uwanja wa mapambano)
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, fuhara ya moyo wako
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2025
Album : (Single)
Added By : Farida
SEE ALSO
AUTHOR
ZABRON SINGERS
Tanzania
Zabron singers is an evangelism group found in Kahama Tanzania, since 2006 to 2015 more than sixty h ...
YOU MAY ALSO LIKE