Home Search Countries Albums

Dawa ya Corona

STEPHEN KASOLO

Dawa ya Corona Lyrics


Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku tata
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku Yesu
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku tata
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku eeh

Matendo yako Bwana yameshangaza dunia
Maarifa ya mwanadamu umeyafanya upumbavu
Wameshindwa tufanye nini sasa?
Wanahangaika suluhu ni wewe tu

Wameshindwa watafanya nini?
Wamejua kwamba we ndiwe konki konki
Hata waimbaji wamechanganyikiwa
Wameacha kuimba Mungu wanaimba Corona

Wanamuziki wamechanganyikiwa
Wameacha kuimba sifa wanaimba Corona
Wewe ndiwe mwisho, wewe ndiwe konki
Wewe ndiwe Mungu ushukuriwe

Ipo nguvu katika sifa
Dunia sifu utapona
Mataifa sifu mtapona
Mungu wetu ni mwenye nguvu

Tunaposifu tutapona, imba
Marekani imba, imba sifa imba
Kenya imba, imba sifa imba
Bwana atashuka kwa matendo yake

Atajidhihirisha kwa watu wake
Njooni tuimbe, imba
Njooni tuimbe, wimbo ni dawa
Waitaliano jamani njooni tuimbe tupate dawa

Ipo nguvu katika sifa
Dunia sifu utapona
Mataifa sifu mtapona
Mungu wetu ni mwenye nguvu

Tunaposifu tutapona, imba
Kenya imba, imba sifa imba
Tanzania imba, imba sifa imba
Marekani, marekani

Nimekuja kusema na wanadamu mimi
Nimekuja kusema na wanadamu mimi
Lazima mjue Mungu ndiye mwisho
Hata serikali wamechanganyikiwa

Kila siku wanatuambia mambo na Corona
Tumgeukieni Mungu wapendwa tupate uzima
Tumgeukieni Mungu mataifa nawaambia
Tukimgeukia Mungu tutapata kupona
Tukimgeukia Mungu tutapata kupona

Ikiwa watu waitanishwao kwa jina langu
Ikiwa watu waitanishwao kwa jina langu
Watanyenyekea na kuomba
Mimi Mungu nitasikia nitaponya nchi yao
Mimi Mungu nitasikia nitaponya nchi yao

Imekuwaje hata makanisa yamefungwa
Moyo wangu unaomboleza na kulia
Imekuwaje makanisa na yamefungwa (Makosa sana)
Kanisani huko ndo unapata faraja
Pale kanisani huko ndo unapata faraja

Ipo nguvu katika sifa
Dunia sifu utapona
Mataifa sifu mtapona
Mungu wetu ni mwenye nguvu

Tunaposifu tutapona, imba
Mutahi Kagwe imba, imba sifa imba
Kenya yetu ipone, imba, imba sifa imba
Sifa ni dawa, imba, imba sifa imba
Italiano njooni, imba, imba sifa imba
Wote na imbeni, imbeni sifa

Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku tata
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku Yesu
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku tata
Mawiko mawiko mawiko, mawiko maku eeh

Imba, imba sifa imba
Imba, imba sifa imba
Imba, imba sifa imba

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2020


Album : Dawa ya Corona (Single)


Copyright : (c) 2020


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

STEPHEN KASOLO

Kenya

Stephen Kasolo is a Kenyan gospel artist/Minister . He is a christ ambasador and best know for ...

YOU MAY ALSO LIKE