Kumekucha Lyrics
Iyeiyeeaaah
Uwouwouwooooh
Lalalalalalalalalalaaaaaa
Kumekucha waambie
Waskie Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie Ukeketaji nao tuutupilie
Kumekucha waambie
Waskie Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie Ukeketaji nao tuutupilie
Kumekucha Tuwafwate ili kuwaokoa Na kuwakomboa
Kama una mawazo ya zamani Sasa toa
Kumekucha Jifunue blanketi ulilojifunika
Blanketi lililokutia kwenye giza La kuwakeketa
Giza lililowanyima Raha Na urembo wao wa kumeremeta
Kumekucha Amka kabla jamii yetu Itiwe makucha
Tunajua hii ni Mila ya zamani Ila sasa Haina dhamani
Zamani ilikuwa kwao ni hatari Lakini sasa kwa wasichana wetu Ni hatari
Na wanasema Zoa mchele kabla ndege Hawajadona
Hebu ona, Ona maelfu wanavyoangamia Kwa kumwaga damu
Ona magonjwa yanavyozagaa Kwa ukeketaji
Kama bado hujaona Hutaona Ila waambie, Kumekucha
Kumekucha waambie
Waskie Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie Ukeketaji nao tuutupilie
Kumekucha waambie
Waskie Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie Ukeketaji nao tuutupilie
Mnavyozidi kuwakeketa
Ndivyo jamii yetu inazidi kuchomeka
Tunavyozidi kuwalazimisha wao kuoleka Kwa wazee waliozeeka
Ndivyo jamii yetu inazidi Kubomoka tulikoezeka
Simama Leo Kuwa mwangaza unaoangaza
Kwani, Taa huwashwa ili kuwekwa peupe Kumekucha
Tazama uzazi unavyokuwa kazi
Tazama magonjwa kama Fistula Yanavyotisha kuwala
Kumekucha Machozi yao kwangu Nikama kwaruzo la pini kwenye ini
Damu yao itaturudia Kama mizimu ndotoni mwetu
Uwepo wao utatoka Vijijini mwetu Najua jamii zetu
Na tamaduni zetu Ni tamu kama asali
Lakini kunazo ambazo Zina uchungu Wa pilipili Kumekucha
Leo ni Leo (Kumekucha )
Leo ni Leo (Kumekucha )
Leo ni Leo ooooh (Kumekucha ) (Kumekucha )
Leo ni Leo (Kumekucha )
Leo ni Leo (Kumekucha )
Leo ni Leo (Kumekucha
Tuungane nchi na nchi Gambia
Hadi Zambia Tanzania wenye nia Libya walete sura mpya
Nigeria na Algeria Maanake Pamoja tunaweza kumaliza ukeketaji
Wa mtoto wa kike Leo ni Leo Kumekucha
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2024
Album : (Single)
Added By : Kunta Kinte
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE