Wimbo wa Taifa Kenya (Swahili) Lyrics
[Stanza 1]
Ee Mungu nguvu yetu
Ilete baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi
Natukae na undugu
Amani na uhuru
Raha tupate na ustawi
[Stanza 2]
Amkeni ndugu zetu
Tufanye sote bidii
Nasi tujitoe kwa nguvu
Nchi yetu ya Kenya
Tunayoipenda
Tuwe tayari kuilinda
[Stanza 3]
Natujenge taifa letu
Ee, ndio wajibu wetu
Kenya istahili heshima
Tuungane mikono
Pamoja kazini
Kila siku tuwe na shukrani
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 0
Album : Wimbo wa Taifa Kenya (Swahili) (Single)
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
KENYA
Kenya
Kenya is a country in East Africa with coastline on the Indian Ocean. It encompasses savannah, lakel ...
YOU MAY ALSO LIKE