Home Search Countries Albums

Imani Lyrics


Yesu wakati mmoja na wanafunzi wake
Yesu wakati mmoja na wanafunzi wake
Akawa amewaamuru kufanya miujiza
Kuponya magonjwa, kutoa mapepo kwa jina lake

Kwa bahati mbaya walikuja na habari mbaya
Wakamwambia Yesu tumetumia jina lako
Lakini kuna huyu pepo ambaye hakutoka
Tukang'ang'ana kwa muda mrefu tukitoa huyu pepo
Tukitumia jina lako Yesu

Yesu akawaambia ole wenu nyinyi wenye imani ndogo
Ole wenu
Kuna mambo hayawezi kufanyika
Pasipo kufunga na kuomba mwenzangu

Katika jina la Yesu simama na unyanyuke 
Katika jina la Yesu amini jina lake 
Katika jina la Yesu simama na unyanyuke 
Kwa imani

Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda
Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda

Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda
Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda

Wanadamu sisi tuna shida moja
Niruhusu niwaambie tusaidike
Mungu anaweza kukutoa katika shimo
Shimo la matatizo makubwa
Shimo ambalo ungeambiwa ungetoka ndani
Ungelikataaa

Nenda ukamwamini Mungu wako
Akakutoa ndani ya shimo
Ukamwamini Mungu wako
Akakusaidia ukasimama 

Hivi kesho unajaribiwa tu na kitu kidogo
Hata lile Mungu alikutoa ndani lilikuwa kubwa
Tena unasahau unaanza kusononeka
Mwezangu kumbuka lile alilokufanyia 

Katika jina la Yesu simama na unyanyuke 
Katika jina la Yesu amini jina lake 
Katika jina la Yesu amini neno lake
Kwamba unaweza yote katika Kristo akutiae nguvu ee

Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda
Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda

Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda
Imani nachembea haradali
Ndio imani inayozaa matunda

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2021


Album : Imani (Single)


Copyright : (c) 2021


Added By : Huntyr Kelx

SEE ALSO

AUTHOR

EVE BAHATI

Kenya

Eve bahati Yaa  is a gospel artist from Kenya. Eve Bahati is a born again worshiper,s ...

YOU MAY ALSO LIKE