Home Search Countries Albums

Kesho Lyrics


Okay
Wanasema tomorrow is the mystery
Wanasema tomorrow
Leo zawadi ikumbatie, jana ni History
Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hii
Wanasema tomorrow is the mystery
Wanasema tomorrow
Leo zawadi ikumbatie, jana ni history
Ya jana hayawezi yaka

Ah Kesho nafasi ya kuanza upya
Kumaliza kuishi nafasi ya kuanza kufa
Kuivunja sheria nafasi ya kufata ruksa
Kuikumbuka jana au kuanza kuifuata future
Future ni leo siku ambayo miti hukimbia
Jua hushuka upendo wa marafiki hufifia
HUFIFIA wimbi la wanafiki huingia
Kesho ya tumaini hubakia
Tumaini shika walau shika walau
Na ujifunza kuziba kombe pindi anapopita nyang'au
Akishapita tenda wema alafu kisha sahau
Na uchunge unaponena watakuzika wadau
Wadau walikuwa uchi ukawavika mavazi
Nyumba yako ikavunjika wakakunyima hifadhi
Je utasamehe utasahu kulipa kisasi?
Au kesho itakukuta umeshika risasi?

Risasi nawaza wapi itakukutisa kesho
Utatoroka kambi ama utavungia Ghetto
Tusipofikia lengo utahama ukoo kwa kitu kidogo
Au utaiitumikia nembo?
Nembo ya mjeshi ninayekaza mwendo kishujaa
Kama unavyoza nyonga kwenye tendo la zinaa
Napiga goti nashukuru uwepo wa sanaa
Kihisia nawapeleka kesho majamaa
 Majamaa walikuwa wavivu hawakukazana
Waliishia kuamini kuwa kuna wingu la laana
Wali-set mipango ila siku hazikufanana
Huwezi kuikabili kesho kwa  mbinu za jana ah

Wanasema tomorrow is the mystery
Wanasema tomorrow
Leo zawadi ikumbatie, jana ni History
Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hii
Wanasema tomorrow is the mystery
Wanasema tomorrow
Leo zawadi ikumbatie, jana ni History
Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hii

Nakuwekea Logic penye Faith
Nakutazama ukishahama nakuwekea topic kai-debate
Ninakunyima msosi kwenye Plate
Njaa ya kesho ikufunze kuheshimu pochi yenye pay
Pay huna unatia neno kwenye bao
Ukirudi unalalama kuhusu kesho ya wanao
Myahudi ukisujudu kwenye uwepo wa Farao kwa wayahudi
Utaishia kwenye Tempo ya karao
Karao kazikwa kama Historia ilivyozikwa na jana
Kesho ni siku ya kujitwika lawama
Kesho ni mbali natumai nitafika salama
Najipa moyo kisha ninaibusu picha ya mama
Mama sishiki simu wakati na-drive sitii vocha
Na mafuta full tank kwa gari sisikii uwoga
Big G za kutosha, Chupa za maji na Diclopa
Na Cd za muziki wa Papii kocha
Kocha kasema Kesho inataka bidii tosha
Nawaeleza watu wangu na bado hawasikii hoja
Wamesahau kesho ni nini, Niliwaamini leo najuta
ila kesho sirudii kosa
Kosa ni kuchoka maana akili haifikiri
Taswira ya kesho naiona na mboni hazihimili
Kelele zimeshamiri masikio yameshagota na
Na mdomo unaropoka, Dunia haina siri
Siri ikasambaa viganja vikanakiri
Miguu ikalemaa ila ubongo ulikariri
Tumbo halikujaa na mwili haukunawiei
Kesho ifike mapema inikute nipo Kamili

Wanasema tomorrow is the mystery
Wanasema tomorrow
Leo zawadi ikumbatie, jana ni History
Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hii

Enjoy Synced Lyrics With Our Mobile App

Download on Google PlayGet it on App Store

WATCH VIDEO

ABOUT THIS SONG


Release Year : 2023


Album : The Verteller (Album)


Added By : Farida

SEE ALSO

AUTHOR

DIZASTA VINA

Tanzania

Dizasta Vina  (real name Edger Vicent) aka "The Black Maradona" is  Hip-hop arti ...

YOU MAY ALSO LIKE