Amelipa gharama Lyrics
Mwanaume huyu Yesu aliaibishwa sana
Pale msalabani ili tupate wokovu
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Kapigiliwa misumari, mijeledi alipigwa
Kwa ajili yetu sote tumeupata wokovu
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Walimtukana Yesu, wakamdhalilisha
Nguo walimvua ili tupate wokovu
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Walimnywesha siki, mate walimtemea
Taji ya miba kichwani ili tupate wokovu
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Walimhukumu Yesu bila kosa lolote
Lengo lao kuzuia injili isihubiriwe jamani
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Alisingiziwa uongo hakujibu lolote
Alinyamaza kimya ili tupate wokovu
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Kama wewe ni mwana wa Mungu, shuka msalabani
Uliokoa wengine leo jiokoe mwenyewe
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Walimtukana Yesu, wakamwita mjanja
Walimtesa sana leo kashinda mauti aah
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Kati ya Yesu na Baraba afunguliwe nani?
Wote wakaitikia afunguliwe Baraba
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Wakamzika kaburini walijua wamemkomesha
Lakini siku ya tatu akafufuka aah
Amelipa gharama huyu Bwana Yesu
Pale msalabani ametuletea wokovu
Huyu Yesu ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Ameshinda kifo na mauti (Ametuletea wokovu)
Amefufuka na utukufu (Ametuletea wokovu)
Yesu kristo yu hai (Ametuletea wokovu)
Bwana Yesu yu hai leo (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Kaburi halikumweza (Ametuletea wokovu)
Kaburi halikumshikilia (Ametuletea wokovu)
Kuzimu imetetemeka (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Yesu ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Yesu ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Kuzimu haikumweza (Ametuletea wokovu)
Mwanaume wa wanaume kashinda kifo (Ametuletea wokovu)
Amefufuka mwokozi eeh (Ametuletea wokovu)
Kule kupigwa kwake tumepona (Ametuletea wokovu)
Kuteseka kwake tumepona (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Kwa kupigwa kwake tumepona (Ametuletea wokovu)
Kwa kupigwa kwake tumekuwa wazima (Ametuletea wokovu)
Kwa kupigwa kwake tunapendana (Ametuletea wokovu)
Ametuweka mbali na laana (Ametuletea wokovu)
Ametuweka mbali na magonjwa (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
Ametuletea wokovu (Ametuletea wokovu)
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2020
Album : Amelipa gharama (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE