Sawa Lyrics
Niliambiwa filisiko ju ya tabia ya mkeo
Na sikuamini nilijua jana si leo
Ningekuwa mchawi ningekufuata kwa uteo
Iyee
Laiti kama ningejua unanifanya chujio
Hata hapana ningelibadili nia
Kiporo cha jana nikakufanya chajio
Iyee
We na labda kuna mabaya niliyofanya
Ila kumbuka na mema niliyofanya
Mwenzako nilizibeba lawama
Ningeyajua machafu katu singezama
Laiti kamwe ningeyatambua haya
Huenda ningeepuka ubaya
Siamini leo ndo langu linazama
Na ndoana nilotupa ndo imekwama
Sawa, sawa tumeamua haya
Sawa, sawa sitalipa ubaya
Sawa, sawa tumeamua haya
Sawa, sawa sitalipa ubaya
Nakumbuka mama nilisema
Mwanangu kuwa uyaone
Ya watu kamwe usije kusema
Ya moyoni yasema
Kumbe ulinipendea gari ile mingi misele
Nikipiga simu unasema kelele
Umenibadilisha jina unaniita kengele eeh
We na labda kuna mabaya niliyofanya
Ila kumbuka na mema niliyofanya
Mwenzako nilizibeba lawama
Ningeyajua machafu katu singezama
Laiti kamwe ningeyatambua haya
Huenda ningeepuka ubaya
Siamini leo ndo langu linazama
Na ndoana nilotupa ndo imekwama
Sawa, sawa tumeamua haya
Sawa, sawa sitalipa ubaya
Sawa, sawa tumeamua haya
Sawa, sawa sitalipa ubaya
WATCH VIDEO
ABOUT THIS SONG
Release Year : 2021
Album : Sawa (Single)
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
SEE ALSO
AUTHOR
YOU MAY ALSO LIKE